Featured
Loading...

Ruby: Namuonea hurama Diva, namwombea kwa Mungu amrudishie akili zake!


Baada ya mtangazaji wa Clouds FM, Diva kudai kwamba hamjui msanii wa muziki Ruby, Ruby ameendelea kutema cheche kuhusiana na kauli hiyo.

Muimbaji huyo ambaye ameachana na uongozi wake wa zamani wa THT, ameonyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Diva na kila akiulizwa kuhusu kauli hiyo amekuwa akitoa maneno makali.

“Kuhusu Diva, bora tu niachane naye maana sioni vitu vya kumuongelea kama anavyofanya yeye,” Ruby aliliambia gazeti la Mtanzania “Zaidi namuonea huruma tu, namsikitikia na ninamwombea kwa Mungu amrudishie akili zake. Nahisi ana ugonjwa wa kusahau, jambo ambalo ni baya sana kulingana na umri wake,”

Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa amefunga ukurasa wa kuzungumzia masuala ya uongozi wake uliopita kuhu akidai kwa sasa ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kimuziki.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top