Inahitajika nidhamu ya hali ya juu sana kifikra na kimaamuzi,
kutoyumbishwa na habari zinazovuma kila kukicha katika taifa letu kwa
sasa. Juzi UKUTA, jana kupatwa kwa jua, leo noti mpya kuchapishwa, kesho
mtu kakamatwa kwa kumtukana Rais, hujakaa sawa mara wanafunzi hewa!
Ukiamua kukisemea kila kinachosikika utajitia "stress" zisizo na sababu
na utapoteza uelekeo. Huu ndio wakati unaohitaji kujipambanua na
kujidhibiti, kwa sababu kinyume na hapo unaweza kugeuka mbwa
unaehangaishwa na mifupa inayorushwa kila siku.(tena mingine kwa
makusudi kukupoteza na kutafuta huruma zako). Ndio maana kwa sasa
nimeamua kutohangaika kabisa na taarifa za habari hasa za kwenye TV!
Kila siku ninashangilia maisha (huwezi kunikuta nikilalamika hata kwa
bahati mbaya), kwa sababu ninajua(kwa uhakika kabisa) kwamba mabadiliko
yamelifikia taifa kwa ajili ya manufaa yangu! Full stop! Mengine wanajua
wenyewe wanaohusika nayo, hayanihusu!
#SmartMind
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )