Fedheha kubwa zaidi inayowakumba mastaa wa wengi wa Bongo Flava ni kutokujua kuongea Kiingereza.
Shilole hataki tena kudharauliwa na ndio maana amedai kutafuta mwalimu wa kumnoa lugha hiyo.
“Mimi nataka nisome kwa furaha yangu mwenyewe ili nijuwe ‘it’s no’ ‘how am doing’ ‘how am speaking’ hicho kitanisaidia sababu kama hela ninazo,” Shishi aliiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM.
“Mimi sitaki kusoma English ili nipate hela cause I have money, nataka tu niweze kurashiarashia hata nikikutana na akina Beyonce nisipate shida.”
Amesema tayari ameshaanza kozi hiyo na kwamba kuna mabadiliko makubwa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )