Featured
Loading...

Wema Sepetu na Idris Sultani Bado Ngoma Nzito...Ampigia Chapuo Kevin Hart MTV Mama Badala ya Idriss


Adui yako muombee njaa – Wema Sepetu na Idrs Sultan ngoma bado ngumu.

Wema amepigilia msumari wa moto kwa kupost picha ya mchekeshaji wa Marekani, Kevin Hart ambaye anawania nafasi ya kuhost kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu na Idris Sultan kama mwanaunme anayempenda #MCM (Man Crush Monday. “MCM….😏😏😏,” ameandika Wema kwenye picha hiyo.

Kitendo hicho cha madam Sepetunga kimetafsiriwa ni kama anampigia chapuo mchekeshaji huyo wa Marekani kushinda nafasi hiyo na kumponda kiaina ex wake, Idris.

Hivi karibuni wawili hao walionekana mahusiano yao kuingia doa na Idris akijikuta akiifunga akaunti yake ya Instagram kwa muda baada ya kuambulia matusi kutoka kwa watu wanaojiita ni Team Wema.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top