Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, Dkt. Wilbroad Peter
Slaa, amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Balozi
wa Tanzania na kusema kuwa yuko tayari kutoa mchango wake katika
kulijenga taifa la Tanzania.
“Kwa
sababu Ubalozi uko kwenye Idara za moja kwa moja za mkuu wa nchi, na
bila shaka hakukuwa na sababu mkuu wangu kutotaka kuniteua, ninamshukuru
kwa uteuzi huo kwa kuniona, ninachoweza tu kusema katika hatua hiyo ni
kwamba ninao wajibu mkubwa hasa katika kipindi hichi cha kulijenga taifa
letu,” amesema Dkt. Slaa.
Dkt.
Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
na ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama hicho,
alijiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na
kuondoka nchini.
Muda
mfupi baadaye Dkt. Slaa alitangaza kutojihusisha tena na siasa za hapa
nchini na akawa anaishi nchini Canada pamoja na mpenzi wake Josephine
Mushumbusi.
Dk.
Slaa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo,
tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015 aliweka wazi
kuwa anafanya kazi zaidi ya mbili ili aweze kujipatia kipato
kitakachomuwezesha kumudu gharama za maisha nchini humo.
Alitaja kuwa kwa sasa anafanya kazi ya Mshauri wa Mauzo (sales Advisor) pamoja na kutoa ushauri (consultancy).
“Mimi
ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza
masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi
ina members (wanachama) 10,000. Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya
5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.
Kufuatia
uteuzi huo wa Dkt. Slaa kuwa Balozi uliofanywa na Rais Magufuli,
taaarifa kutoka ikulu imeeleza kuwa zoezi la kuapishwa kwake litafuata
baada ya kukamilishwa kwa taratibu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )