Chama
tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, kimemtimua Rais Robert Mugabe, kwenye
uenyekiti wa chama na kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais kabla ya kufutwa
kazi na Mugabe, Emerson Mnangagwa kuongoza chama hicho.
Anatakiwa
ajiuzulu mwenyewe urais au kung’olewa madarakani kwa lazima kwa
kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la nchi hiyo.
Vilevile
chama tawala ZANU-PF kimemfutia uanachama mke wa Rais Mugabe, Grace
Mugabe. Hatua hiyo inamnyang’anya moja kwa moja cheo cha uenyekiti wa
Baraza la Wanawake la chama hicho.
Washiriki
wa karibu wa Rais Robert Mugabe katika chama alichokianzisha wamemtaka
kiongozi huyo kuondoka madarakani kufuatia shinikizo kubwa la maandamano
linaloendelea nchini humo sanjari na jeshi kuingilia kati.
Katika
kikao hicho kinachoendelea leo, Novemba 19, viongozi wa juu wa chama
hicho wanalenga kuzungumza iwapo wamuondoe kiongozi huyo kwenye chama
ama la huku umoja wa vijana wa chama hicho ambao walionesha kuwa watiifu
kwa kiongozi huyo na mkewe muda wote nao wakimgeuka.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )