Mahakama
ya rufaa nchini Afrika Kusini imemuongezea adhabu ya kifungo
mwanariadha mwenye ulemavu Oscar Pistorius kutoka miaka 6 hadi miaka 13
na miezi mitano kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hatua hii inafuatia madai kutoka upande wa serikali kwamba adhabu aliyopewa awali ya miaka sita ilikuwa ndogo.
Hatua hii inafuatia madai kutoka upande wa serikali kwamba adhabu aliyopewa awali ya miaka sita ilikuwa ndogo.
Pistorius
alishtakiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi 4, katika siku ya
wapendanao mwaka 2013, na baadaye Pistorious alisema alifyatua risasi
hizo kwa kujua ni mwizi.
Familia ya Reeva Steenkamp imeeleza kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa mahakama na inaonesha kuwa haki inaweza kuendelea kutendeka nchini humo Afrika Kusini.
Familia ya Reeva Steenkamp imeeleza kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa mahakama na inaonesha kuwa haki inaweza kuendelea kutendeka nchini humo Afrika Kusini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )