Mwanamuziki
na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba
ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa
la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja
ya kuendelea na 'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba
hai.
Patcho
ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba
amesema kwamba Mama kanumba anapaswa kuwa na moyo wa kusamehe kwa
sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na
maisha yake hivyo kujengeana chuki siyo jambo jema.
"Sina
la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama
ilivyoamua, kwa upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa
miaka miwili ni bahati, ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela
siyo sehemu nzuri sana kwa mtu kuwepo kila mtu anajua hilo hasa
ukizingatia bado ni mdogo hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu, uwezo
naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.
Aidha
Patcho ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki
imetendeka, mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye,
ambaye pia ni rafiki yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya
Mungu. Hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda
kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna haja ya kuendeleza ma beef japo
yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea vizuri?. Sidhani yule mama
yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".
Patcho
amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu
sidhani ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu
hakumuua Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa ndichi
ninachokiamini. Baadaye Lulu atatoka jela je ukimuon utamgonga na gari?
au Mama Lulu utaweza kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja.
Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )