Waumini
wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange,
Miono, Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ,wamemshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa
zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia
pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka
Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti
huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha
Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.
Mara
baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais
Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo
lililokusudiwa.
Akiungumza
mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba
ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombil lao
la kupata zulia, na kwamba kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais
amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila
katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Sheikh
Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea
kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao
kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani
anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi
wote.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pwani
17 Novemba 2017.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )