Mbunge
wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amefunguka na
kusema ahadi ambazo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakipewa
jambo linalopelekea kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lema
amesema hayo jana Disemba 14, 2017 mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la
Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel kutangaza kujiuzulu nafasi
yake ya Ubunge na uanachama wa CHADEMA kuanzia jana na kujiunga na
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Nitakupa
mshahara wako wote kwa miaka iliyobaki, pia nitakulipia madeni yako
yote, nitakupa kiinua mgongo chako chote nitakupa na mlinzi kwa kipindi
hiki na ukitaka tena kugombea nitakupa kipaumbele wewe au kazi nyingine
utakayotaka? Je, utakuwa tayari? Si utakuwa tiyari wajameni?" aliandika Lema kwenye mtandao wake wa Twitter
Baadhi
ya vyama vya upinzani nchini vimekuwa vikikumbana na changamoto ya
baadhi ya viongozi wao au wananchama kujivua uanachama na kujiunga na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai wanaunga mkono juhudi na
utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )