Katibu
wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Humphrey Polepole
amevipiga kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya
vyama hivyo kusema hela ziko wapi.
Kupitia ukurasa wake wa “Twitter” Polepole amendika maneno hayo bila kufafanua ni mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku.
Mbali
na hilo Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa
upinzani hawataweza kushindana na chama chake siku za baadaye kimeanza
kutimia.
Hii
inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe
ambaye hivi karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo
wa Ubunge endapo Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi
kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika
mwezi Novemba mwaka huu.
“Nalipata
kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye
imekuwa. Kwa lugha ya shule ya msingi miaka ile ningesema "wameogopa
kuputa", wangeputa waone namna ambavyo kwetu siasa za masuala zinalipa.
Ushauri wangu: "Mwenyekiti" lazima aseme hela ziko wapi”, ameandika Polepole.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )