Mahakama
ya Hakimu Mkuu mkazi Kisutu imekataa kuyafuta mashtaka 20 ya
utakatishaji fedha kati ya 43 yanayomkabili aliyekuwa mhasibu wa
TAKUKURU Godfrey Gugai na wenzake na kusema kuwa mashtaka hayo kwa sasa
yana nguvu kisheria.
Akitangaza
uamuzi huo wa mahakama Hakimu Mkazi Kiongozi Thomas Simba amesema
uamuzi wake huo unahitimisha mjadala aliouahirisha aliposikiliza kesi
hiyo kwa mara ya kwanza Novemba 16 kama je mashtaka ya utakatishaji
fedha katika hati ya mashtaka ya Gugai na wenzake yaendelee au la.
Mara
baada ya kutoa maamuzi hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi
Desemba 18 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili
Vitalis Peter kusema kuwa upelelezi haujakamilika ambapo watuhumiwa
wanatetewa na wakili Alex Mgongolwa.
Godfrey
Gugai na wenzake watatu walifikishwa katika mahakama hiyo ya Kisutu
wakikabiliwa na makosa 43 ikiwemo kutakatisha fedha,udanganyifu pamoja
na umiliki wa mali nyingi kwa Gugai kinyume na kipato chake halisi
ambapo makosa mengi yanamhusu Gugai pekee yake.
Kutokana
na uamuzi uliotolewa safari hii na Hakimu Simba Washtakiwa wote
wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka wanayokabiliwa nayo,ya
utakatishaji fedha,hayana dhamana na kesi yao itasomwa tena mahakamani
hapo Desemba 18.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )