Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John
Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye
upendo wa aina yake.
Mrema
amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya
ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.
“Namvulia
kofia kabisa, huyu ni Rais msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa
Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”
Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.
“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”
“Nilianzisha
kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini
kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai
kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa
magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao
wanatakiwa kutoka,”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )