Uchaguzi
wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) ambao ulikua ufanyike jana
umesogezwa hadi leo kupisha mashauriano yatakayofanywa na baraza la
mawaziri wanachama wanaohusika moja kwa moja na Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC) baada ya mbunge kutoka Uganda, Freddy Mbidde kupinga
Tanzania kuwa na mgombea.
Chanzo
cha mgogoro huo kinadaiwa ni Tanzania kuwa na mgombea wa nafasi ya
Uspika, Adam Kimbisa wakati nafasi hiyo huwa ni kupokezana na Spika wa
kwanza wa Eala, Abdulrahman Kinana alitoka Tanzania akifuatiwa na Kenya
kisha Uganda.
Mbidde
ametoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge kutokana na akidi kutotimia wakati
wa kufanya uchaguzi licha ya wabunge kutoka nchi zote sita kula kiapo
cha utii mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete.
Baadaye
ilibainika wabunge wengi wa Tanzania na Burundi hawakuwemo kwenye
ukumbi wa bunge na Mbidde kuomba kutoa muda wa mashauriano zaidi ili
kuruhusu nchi zinazostahili kuwa na wagombea kufanya hivyo ambazo ni
Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
Hata
hivyo hadi jana wagombea wa nafasi hiyo walikua watatu ambao ni Adam
Kimbisa, Leontine Nzeyimana ambaye ni Waziri wa zamani Afrika Mashariki
wa Burundi na Mwendesha mashtaka Mkuu mstaafu wa Rwanda, Dk Martin Ngoga
huku Sudani Kusini ambaye ni mwanachama mpya katika jumuiya hiyo
haikutoa mgombea.
Katibu
wa Bunge, Kenneth Madete aliahirisha bunge hadi leo saa 8:30 mchana
kwaajili ya kumchagua Spika na baadaye makamishna na kuunda kamati
mbalimbali zitakazosaidia kutekeleza majukumu ya bunge hilo la nne.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk Suzane
Kolimba amekiri kuwa baraza la mawaziri watakutana kushauriana ni njia
ipi itumike kabla ya uchaguzi wa kumpata Spika wa nne.
"Kumetokea
kutokuelewana na sisi baraza la mawaziri tutakutana kushaurina namna ya
kusonga mbele katika hali hii na uchaguzi utafanyika kama mnavyojua
suala la akidi ni muhimu katika vikao vya wabunge," alisema Kolimba
Awali
wabunge tisa kutoka nchi sita wanachama wa EAC ambazo ni Kenya,
Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini waliapa kuwa wabunge
katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika
uzinduzi huo Mwenyekiti wa bunge la Tanzania, Azzan Musa Zungu
amemwakilisha Spika wa Bunge, Job Ndugai pia walikuwepo Spika wa bunge
la Senate la Kenya, Ken Lusaka .Spika wabunge la Senate ya Rwanda,
Banard Mukuza, Spika wa bunge la Sudani Kusini, Anthony Makana.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )