Shamsa Ford. STAA wa Filamu nchini,
Shamsa Ford amefungukia uamuzi wa msanii mwenzake wa Muziki, Zuwena
Mohammed maarufu kama Shilole kwa kuamua kufunga ndoa tena ya Kidini na
mpenzi wake, Uchebe ndoa iliyoshuhudiwa hivi karibuni na kutikisa kwenye
mitandao na vyombo vya habari huku ikiwaacha midomo wazi kwa wale
walidhani kuwa angerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda.Shamsa
ambaye pia alifunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake, Chidi Mapenzi
ametumia ukurasa wake wa Instagram kumsihi Shilole atulie, aweke
umaarufu pembeni, aitunze ndoa yake na hatimaye atafaidi matunda ya ndoa
iliyo bora. Shamsa ameandika;“Hongera
sana mamy. Umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.Cha
muhimu uwe mke bora wa Kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni.
“Mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana inshaallah
mtazikana.Karibu kwenye Chama mama….Sasa nyie mnao subili matajiri
wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubili
sana mpaka uso uote sugu.Uzuri na Ustar una mwisho wake. Iitafika muda
hata inzi hakusogelei……HONGERA MAMA @shilolekiuno_badgirlshishi,”
ameadika Shamsa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )