BAADA ya hivi karibuni kufunga ndoa na
Ashraf Uchebe, msanii wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungukia
tetesi za kuwa amemchukua mume wa mtu na kusema siyo za kweli. Akipiga
stori na Risasi Vibes, Shilole alisema mumewe hana mwanamke mwingine na
hajawahi kuoa bali yeye ndiye mkewe halali hivyo wanaosema kwamba ana
mke ni waongo, anachomshukuru Mungu ni kwamba anafurahia ndoa yake na
mambo yanaenda vizuri. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install
#GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia
sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee! “Maisha ya ndoa ni mazuri sana
tofauti na kipindi sijaolewa, kilichobadilika ni kwamba kila kitu
ninacho-kifanya lazima nimshirikishe mume wangu kuhusu wanaosema ana
mwanamke mwingine ni waongo kwani hajawahi kuoa na hakuna mwingine zaidi
yangu,” alisema Shilole.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )