Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu ameeleza kuwa kwa saa hali
yake imeimarika sana huku akiendelea na mazoezi ya viungo kutokana na
kujeruhiwa sehemu kubwa ya mwili wake.
“Hali
yangu ya Afya abado inaendelea vizuri,Bado niko Hospitali mguu wangu
unauona uko juu maana yake ni kwamba sijapona kabisa, nimevaa nguo za
hospitali maana yake bado ni mgonjwa. Lakini niwaambie watanzania pamoja
na wananchi wengine wote ambao wamefuatilia afya yangu tangu tarehe 7
septemba, kwamba naendelea vizuri sana,” alisema Tundu Lissu.
Tundu
Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba
7, nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma, ameeleza kuwa kwa sasa hana
jeraha lolote la risasi na hali yake ni nzuri kuliko awali huku akitaja
kuwa bado ana risasi moja ndani ya mwili wake ambayo haijatolewa.
“Hivi
tunavyozungumza sina jeraha lolote la risasi. Risasi 16 ziliingia
kwenye mwili wangu na 7 zilitolewa na madaktari hapahapa, na moja bado
iko kwenye mwili wangu. Lakini sina majeraha yoyote ya risasi. Hali ni
nzuri kuliko nilivyoletwa, nililetwa vipande vipande kabisa,” alisema
Lissu.
Akizungumzia
vuguvugu za kisiasa zinazoendelea nchini kwa sasa ikiwamo kuhama hama
kwa baadhi ya wanachama wanaojitoa katika vyama vyao na kuhamia vingine,
Lissu alisema kuwa hilo halitishii kwa namna yoyote ile uhai wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwani wapo watu wengi sana ambao
wamehama chama hicho na bado kinaendelea na harakati za kiukombozi.
“Mbunge
wa kwanza kabisa wa CHADEMA katika historia ya vyama vingi ya nchi yetu
anaitwa Amal WAlim Kabur, ndiye alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa
CHADEMA, na mimi nilipojiunga miaka 14 iliyopita, alikuwa Makamu
Mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa CHADEMA Kigoma Mjini, alihamia CCM
baada ya kuhamia CCM CHADEMA ilikufa?… Mzee Said Arth Mbunge wa Mpanda
Mjini, alirudi CCM, CHADEMA ilikufa?, Dk Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA
kwa vipindi vitatu mfululizo, baada ya safari kuwa ndefu mno, akashukia
njiani, CHADEMA imekufa?…” alihoji Lissu.
Mbunge
Tundu Lissu alieleza pia kuwa kukaa kitandani ndani ya Hospitali kwa
muda wa miezi mitatu sasa kunamfanya ‘aimiss’ kazi yake ya Ubunge, kwani
ndiyo kazi anayoipendelea zaidi.
“Mimi
napenda Ubunge, yale mapambano ya mule ndani, mapambano ya kiitikadi,
kisiasa. Unamkaba Waziri Mpaka anakosa pa kukimbilia. Hiyo ndiyo kazi
ninayopenda mimi. Na kwa hiyo hakuna kazi ninayoimiss mii kama kazi ya
Ubunge Bungeni..” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )