Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini, Sudi Mussa Mpiri
atafanyiwa uchunguzi kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo
kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Agizo
hilo la kufanyiwa uchunguzi limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Selemani Jafo, ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa
mkurugenzi huyo baada ya kutoridhishwa na miradi ya maendeleo
aliyoitembelea.
Mussa
Mpiri anadaiwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na
Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani. Imeelezwa
pia zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya pesa hizo hayafahamiki hivyo
kutia shaka juu ya utendaji wake.
Kufuatia
hatua hiyo Waziri Jafo, ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji
kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka ndani ya Halmashauri hiyo
kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa Mkurugenzi huyo.
Jafo
amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa
niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia
rasilimali za Halmashauri hiyo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )