Mbunge
Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana
kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo
la Katoliki, Rulenge Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi.
Wabunge
hao kwa nyakati tofauti wameeleza hisia zao juu ya jambo hilo na kudai
watu wanaofanya jambo hili ni wazi hawana hofu ya Mungu lakini pia ni
njia ya kuwatisha watu hususani wale ambao wanakuwa wanaikosoa serikali.
"Najuai
inavyokuwa unapoambiwa ama kuanza kujazishwa fomu na kuhojiwa juu ya
Uraia Wako ni kama kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba
yako. Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata hofu
ya Mungu" aliandika Hussein Bashe
Hata
hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema
kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao
wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali
inakuwa inafanya.
"Baba
askofu pole sana. Kuna watu wakubwa tu kwenye Taasisi nyeti wanaamini
kwa ushahidi kuwa aliyeagiza uhojiwe mwenyewe sio raia wa Tanzania.
Suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya wakosoaji wa Serikali. Ni
ushamba" alisisitiza Zitto Kabwe
Askofu
Severine Niwemugizi amesema kuwa amehojiwa kuhusu uraia wake mara
mbili. Mara ya kwanza aliitwa kwenye ofisi za uhamiaji Ngara Novemba 28,
2017 na mara ya pili Disemba 4, 2017.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )