Marekani
iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya
masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex
Tillerson amesema.
Taaarifa
yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea
Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote
kufanyika
Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika.
Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.
Kando
na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu
alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa
Korea Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.
Uhusiano
wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika
kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na
kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na
kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Akizungumza
kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw
Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini
kujihami kwa silaha za nyuklia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )