Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema
zaidi ya dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja
wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
Akiwa
jukwaani mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, Rais
Magufuli ameweka wazi kuwa amepata taarifa zaidi ya kiasi cha dola
bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria kupitia
uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
“Ninapozungumza
tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja dola zimeshikwa
Airport zilikuwa zinaingizwa Tanzania kwasababu Tanzania kimeshaonekana
ni kichaka cha fedha za kigeni” amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande mwingine Rais amezitaka mahakama za biashara nchini kuharakisha
kesi zinazohusiana na kesi za mikopo ili kuwezesha Benki kuendelea kutoa
mikopo. Pia ameongeza kuwa baadhi ya wakopaji hutumia fedha hizo hizo
za mikopo kuchelewesha kesi, hivyo mahakama zinatakiwa kutoa hukumu kwa
wakati.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )