Featured
Loading...

BABU SEYA KUACHIWA HURU NA RAIS KIKWETE


Kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, SURA YA PILI, SEHEMU YA KWANZA, IBARA YA 45, inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, ama bila ya masharti au kwa masharti, au kumwachilia kabisa mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.
Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi la kusamehewa na kuachiwa huru kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tar 20/06/2014.
Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete. Chikawe akijibu ombi hilo alisema “Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top