MAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’! Ni
kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja
aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke
wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz.
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni- Malapa jijini Dar es Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema
familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali
na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Habari zikazidi kudai kwamba, ilifika mahali katika kumtaka shemejiye
huyo ambaye alikuwa akimkatalia katakata, Mwaweje alitumia gia nyingine
ikiwemo ya kumuahidi mambo manono kama angekubali kuivunja amri ya 6 ya
Muumba na yeye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa, ‘Mungu si Athuman wa Lucas’
siku isiyo na jina jamaa alimtumia ujumbe (SMS) mke wa mwenzake kwa
kutumia maneno ya kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo bwana simu alikuwa
nayo mwenye mke.
Chalz alimwita mkewe na kumuuliza ni nani aliyemtumia ujumbe huo? Ndipo mke akaanika ukweli akisema:
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume: “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume: “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”
Za mwizi 40: Bwana Anton John akiwa na pingu mkononi baada ya kunaswa na kamanda wa OFM pamoja na wanausalama.
Pia, mwanamke huyo alimwonesha mumewe meseji kibao ambazo jamaa huyo amekuwa akimtumia na zile ambazo yeye amekuwa akimkatalia.
“Sasa sikia, mkubalie,” mwanaume huyo alimwambia mke wake huku midomo ikimcheza kwa hasira.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )