
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Membe alisema ubalozi huo
unatarajiwa kumpa taarifa mapema iwezekanavyo na leo atatoa taarifa
kuhusu mauaji hayo, yaliyofanywa na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.
“Kuhusu
suala hilo nitatoa taarifa kesho (leo) baada ya kupata taarifa rasmi
kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini humo….na nitajua nitatoa kwa kuita
waandishi au kutuma taarifa tu,” alisema Membe aliyekuwa akitoka katika Misa ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph.
Alisema
hajapata taarifa zozote, lakini ubalozi wa Tanzania nchini humo
unaendelea kufuatilia kama kuna wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa
wakisoma chuoni hapo na kufa au kujeruhiwa.
Chuo
kikuu hicho nchini Kenya kililipuliwa na magaidi wa kundi la Al-Shabaab
na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa huku baadhi ya wanafunzi
hawajulikani walipo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )