Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA
Ilipoishia...
Daktari
aliye kuwa anaendelea kunipiga baada ya kumuona mwenzake akiwa anaaga
dunia akaniacha na kwa nguvu zake zote akarusha kirungu chake na kikatua
kichwani mwa sheila na akadondoka chini na damu za puani zikaanza
kumwagika
Endelea....
Taratiu
nikaanza kujiburuza chini hadi sehemu aliyo angukia sheila huku machozi
yakinimwagika na kujikuta nikijilaza juu yake na kumfanya daktari aliye
mpiga akanza kunipiga tena kwenye mgongo akinimrisha nimuechie sheila
ili aendelea kumshuhulikia kwa kipigo.Kila nilipo jaribu kumtingisha
sheila sikuweza kuona dalili yoyote ya kuishi kwake na kujikuta nikizidi
kumkumbatia kwa uchungu.Nikaanza kusikia makelele yakija kwa nyuma
yangu,nikageuza shingo yangu na kuona kundi kubwa la vichaa wakija kwa
kasi na kumfanya daktari anaye nipiga kutimka mbio na sikujua ni wapi
anapo elekea na wote wakanipita na kuendeleka kumkimbiza dakrari aliye
kuwa akinipiga.
Nikaona
nikiendelea kujiliza haita saidi zaidi ya kumfanya sheila kuzidi
kuzidiwa na kipigo alicho kipata.Nikajikaza na kwabahati nzuri miguu
yangu ina nguvu za kutosha nikanyanyuka na kujinyoosha japo nilijawa na
maumivu makali ila sikuwa na jinsi.
Nikanyanyua
sheila na kutokana na kudhohofika kwake kwa mwili haikuwa ngumu kwangu
kumbeba hadi tukafika kwenye kwenye moja ya ofifisi na kuwakuta vichaa
wakiwashambulia manesi waliomo ndani ya ofisi.Hali ya hospitali
imechafuka kupita maelezo madaktari wanashambuliwa na vichaa ambao
wamepandwa na hasira.Kwa bahati nzuri nikaona gari moja ya waogonjwa
amayo imesimama nje kwenye maegesho huku dereva wake akichomolewa kwenye
gari na kuanza kupewa kipigo kama ilivyo kwa wahudumu wengine wa
hospitali ikiwemo walinzi.
Hapa
ndipo nikagundua kuwa vichaa tunafahamiana kwa maana kwa kila nilipo
pita huku nikiwa nimembeba sheila hapakuwa na anaye nigusa tofauti na
wanapo muona muudumu wa hospitali hii.Nikafanikiwa kufika kwenye gari la
wagonjwa nakumuingiza ndani ya gari sheila na kwenda upande wa dereva
na kuanza kutafuta fungua na sikuweza kuiona ikanibidi nishuke na kuunza
kuupapasa mwili wa dereva ulio lala pembezoni mwa gari na kwabahati
nzuri nikaiona funguo kwenye mfuko wake wa suruali.
Nikawasha
gari na kuondoka hukiwasaidia vichaa kutoka ndani ya hospitali hii
baada ya kuligonga geti lililokuwa kimefungwa.Kutokana sikuwa ni
mwenyeji sikujua ni wapi nielekee ili kumuwahisha sheila
hospitali.Nikasimamisha gari pembezoni mwa arabara huku likiwa linawaka
ving’ora na kuichukua simu iliyopo ndani ya hospitali na kuanza kubuni
namba ya baba
Kwa
mara ya kwanza ikapokelewa na mwanamke ambaye hata lugha hatulewaa na
nikajua nitakuwa nimekosea,nikajaribu kufikiria namba nyingi ambazo
zinaweza kufanana na namba ya baba na pia namba niliyo ipiga ikapokelewa
na kijana na akaanza kumwaga matusi alipoona sizungumzi kitu chochote
baada ya kusema haloo.Nikajaribu zaidi ya mara saba nipo kumbukumbu ya
namba za baba ziliponijia vizuri kichwani na nikaipiga ikaita kwa muda
kisha ikapokelewa
“nani mwenzangu?”
Ilikuwa ni sauti ya baba na kidogo tabasamu likanijia usoni
“mimi eddy”
“eddy……!!”
“ndio ni mimi baba ninaomba msaada wako”
Upo wapi mbona makelele ya king’ora?”
“nipo kwenye gari ya wagonjwa nimetoroka hospitalini ila mimi sio kichaa kama ulivyo dhania”
“ngoja kwanza umesema upo wapi?”
“mimi hapa wala sipajui ila kuna magorofa mafupi mafupi hii na kuna magari mengi yamesimama pembeni”
“umesema upo kwenye gari ya wagonjwa?”
“ndio”
“wewe ndio dereva ua kuna dereva?”
“mimi ndio dereva”
“sasa angalia kwenye upande wa kusoto kuna kijitivii kidogo….”
“ndio nimekiona”
“kiwashe kama hakija washwa na kwenye sehemu ya chini yake kuna batani nane umeziona”
“ndio”
“minya batani iliyo andikwa map”
Nikaiiminya
batani ambayo baba aliniambia na ndani ya sekunde kadhaa kukatokea
ramani yenye mistari mingi mingi huku kukiwa na kialama chekundu kikiwa
kina waka waka
“inakisoma vipi hiyo ramani?”
“inasoema cape town, western cape city”
“subiri tunakuja sasa hivi”
Nikakata
simu na kuzima gari na kufungua kijidirisha kilichopo nyuma ya siti
yanga na kumuona sheila akiwa amejilaza huku akipumua kwa shida kidogo
nikapata matumaini.Ndani ya nusu saa gari mbili zikasimama mbele ya gari
nililipo na mtu wa kwanza kushuka ni baba na moja kwa moja akafika
kwenye gani na akaonekana kunishangaa jinsi damu zinavyo nivuja.Watu
wake wakanitoa ndani ya gari
“baba kuna mtu mwengine huku nyuma”
“ni nani?”
“rafiki yangu”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )