Shabiki
wa soka nchini Bangladeshi ambaye alipoteza miguu yake yote miwili
katika ajali ya treni anasema licha ya kutokuwa na miguu bado ana ndoto
za kuwa mchezaji ambaye atashindana na Cristian Ronaldo.
Mohammad
Abdullah mwenye miaka 22, alipoteza miguu yake miwili kwenye ajali ya
treni miaka kumi iliyopita lakini sasa kijana huyo ambaye pia anafanya
kazi kama mbeba mizigo katika kituo cha kivuko, sasa anatengeneza jina
kwa ujuzi wake wa mpira wa miguu .
Abdullah
alitelekezwa na mama yake wakati akiwa na miaka saba na akawa amelelewa
na baba yake na mama yake wa kambo kabla hajakimbia
>>>’nilikuwa
na hasira na mnyonge, nisiye na msaada , niliishi barabarani na kuomba
msaada na baada ya miezi kadhaa nilipata sehemu ya kukaa na bibi yangu’
Baada ya
ajali kwenye treni alikimbizwa hospitali ambapo alibaki peke yake wala
hakuna mtu yeyote kutoka kwenye familia yao aliyefanya mawasiliano naye.
Hatimaye hospitali ilimpeleka kwenye kituo cha watoto yatima baada ya
yeye kupata nguvu. Kituo kilimpeleka shule ambapo Abdullah anakiri kuwa
alisoma kwa miezi 18 lakini baadaye alikimbia tena
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )