Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ameibua suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji kiaina.
Akichangia
 mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2019/20 bungeni 
leo Jumanne Novemba 6, 2018 , Mchungaji Msigwa alisema wafanyabiashara 
hawako huru kufanya biashara nchini.
“Wawekezaji wanajionaje kuwepo katika nchi hii, wapo salama? Takwimu zinaonyesha wawekezaji wa nje wanafunga virago.
“Je wawekezaji wa ndani wakoje? Wana raha? Kama bilionea mkubwa nchi hii anaweza akashikwa, akafichwa, akaachiwa halafu hadi leo hajaruhusiwa kusema alikuwa wapi unadhani nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? Haya mambo hatuwezi kufumbia macho, lazima tuyajadili.”
“Je wawekezaji wa ndani wakoje? Wana raha? Kama bilionea mkubwa nchi hii anaweza akashikwa, akafichwa, akaachiwa halafu hadi leo hajaruhusiwa kusema alikuwa wapi unadhani nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? Haya mambo hatuwezi kufumbia macho, lazima tuyajadili.”
Alisema hadi leo hakuna taarifa ni nani aliyemteka na pia alikuwa wapi na kuhoji  kwa sasa diplomasia ya nchi ikoje.
“Wakati
 wa Benjamin Mkapa (Rais wa Awamu ya Tatu) aliwahi kusema Tanzania 
inahitaji ulimwengu kuliko ulimwengu unavyotuhitaji sisi.”
“Kama
 leo Balozi wa Ulaya anaitwa nchini kwake kujadili mahusiano  kama taifa
 linahitaji kujiuliza wageni wanaionaje Tanzania. Wafanyabiashara 
wanafunga virago wanaondoka kwa sababu wanaona hawako sawa. Mheshimiwa 
Mpango, (Waziri wa Fedha na Mpango Dk Philip Mpango)  Serikali yako 
haieleweki inaendeshaje uchumi wa namna gani?” alihoji.
Aidha,
 alisema taifa linahitaji Katiba ambayo itawaunganisha Watanzania wote. 
Mwalimu Nyerere walipigana vita ya Uganda na wakashinda kwa sababu 
walikuwa wamoja,” alisema.
Alisema kinachowaunganisha Watanzania wote ni Katiba ili kuweza kupigana na kushinda vita ya uchumi.
Alisema
 wateule wa Rais wanamtii yeye tu na kwamba kila mtu ni kambale (samaki)
 na kwamba wakuu wa mikoa na wilaya hawawatii mawaziri.
“Mtu
 anatumia Instrument (vifaa) vya Serikali amekaa katika ofisi yenye 
bendera, polisi wanamlinda halafu mnasema hayo ni ya  kwake mwenyewe. 
Kama ni ya kwake mwenyewe kwa nini hamchukulii hatua?” alihoji.
Wakati
 akiendelea kuchangia, aliibuka Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel 
na kutaka kufahamu Chadema ilizungumza nini katika kikao walichokifanya 
kati yao na mashoga 40.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge,  Mussa Zungu alimpotezea Dk Mollel na kumtaka Mchungaji Msigwa aendelee kuchangia mpango huo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
 

 
 
 
 
 
 
 
