Polisi
 Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana 
kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.
Akizungumza
 leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Liberatus 
Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata 
wanamfikisha mahakamani.
“Polisi
 tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata
 lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.
Amesema
 kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume 
huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
 

 
 
 
 
 
 
 
