Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeazimia kuwa wabunge wake wote
wanaoshiriki Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) wanatakiwa kuondoka mara moja kwenye kambi ya timu ya Tanzania.
CHADEMA
kimefikia uamuzi huo katika kikao chake cha dharura kinachoendelea
ambacho kiliitishwa kwa lengo la kutafakari kwa kina maendeleo ya hali
ya siasa nchini.
Chama
hicho kimesema kuwa maagizo hayo yameanza kutekelezwa usiku wa
Jumatano, Disemba 6 mwaka huu baada ya kupitishwa kwa azimio hilo ambapo
Kamati Kuu ilimuagiza Katibu wa Bunge kuwafikishia wabunge wahusika
mara moja
Baada
ya kupokea tathmini ya kina ya Uchaguzi wa marudio katika Kata 43
uliofanyika hivi karibuni CHADEMA kimebaini kuwa ulitawaliwa na uvunjifu
Mkubwa wa Haki za binadamu.
Aidha
CHADEMA kimesema kuwa maazimio mengine ya kikao cha Kamati Kuu ambacho
kinaendelea jijini Dar yatatolewa katika hatua ya baadae ambapo umma
utaarifiwa rasmi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )