Mwanamke aliyedaiwa kusahula baada ya kugombana na bwana'ke.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo mbali ya kuwa na mtu wake
amedaiwa kuwa na tabia ya kuchepuka na wanaume tofauti ambapo amekuwa
akifanya hivyo kwa kupanga chumba katika moja ya gesti (jina kapuni)
iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar.
ISHU ILIKUA HIVI
Inadaiwa kuwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanamke huyo kama
kawaida yake alipata mteja ambaye ni mdogo kwake kiumri, ambaye pia ni
mkazi wa eneo kulikotokea varangati hilo.
“Walikubaliana na huyo kijana kupumzika kwa muda na yule mwanamke katika
chumba alichopanga, baada ya kumaliza mambo yao kijana aligoma kumpa
hela ndipo mtiti ulipoanzia,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.
...Akigomba.
ASAULA KUMLAANI
Chanzo kiliendelea kumwaga ubuyu: ”Tulishangaa kuona watu wakivutana
huku mwanamke akiwa na kanga moja, ndipo kijana akapata upenyo na
kuchoropoka na mwanamke yule akaanza kuvua nguo huku akisema anamlaani
kutokana na umri wake kuwa mdogo na kumdhulumu chake.
“Watu walimsihi lakini akawa hasikii zaidi ya kuendelea kuvua na kuamua
kumfuata yule kijana kwao huku akiendelea kuvua njia nzima, alipofika
kwa yule kijana alianza kugonga geti kwa fujo huku akitoa maneno ikiwemo
ya kumlaani.
“Pamoja na makelele na kusaula kote nguo zake lakini hakuambulia kitu
zaidi ya kuonesha sehemu zake za siri na baadaye aliamua kuondoka.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )