Wapiganaji wa kundi la Islamic State wanaimarisha maeneo waliyoyateka nchini Syria na Iraq.
Wameripoti kuliteka eneo la mpakani la mwisho lililokuwa likidhibitiwa na serikali.
Nchini Iraq wanaonekana kuvunja ulinzi wa serikali nje ya Habbaniyah,ambapo wapiganaji wa kishia wanakongamana ili kutekeleza mashambulizi.
Wapiganaji hao wa jihadi wanaelekea mashariki karibu na mji wa Baghdad.
Runinga ya serikali ya Syria inasema kuwa wanajeshi hao walisalimu amri.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )