Watu
saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha mbalimbali za jadi,
wamempora bunduki aina ya SMG askari polisi PC Shadrack.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Mnyambuga alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 2.36 usiku katika ofisi za Kampuni ya Simu za Mkononi
ya Halotel, eneo la Medeli.
“Majambazi
wapatao saba wakiwa na mapanga na nondo walifika katika ofisi hizo
baada ya kutoboa ukuta na kumjeruhi askari kwa mapanga na nondo na
kupora silaha aina ya SMG,” alisema.
Kamanda huyo alisema polisi walifanya msako mkali usiku huo na kufanikiwa kuipata silaha hiyo eneo la Mbuyuni.
“Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na anaendelea kuhojiwa,” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )