Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO
Serikali
kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya takribani Sh.
billioni 12 kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikwepa kodi na kupewa
muda wa siku 14 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kulipa kodi hizo kwenye mamlaka hiyo.
Akitoa
takwimu hizo jana mara baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alisema, kila Mtanzania ana
jukumu la kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na sio kukwepa na amehaidi
kulisimamia vizuri suala la ukusanyaji wa mapato katika sehemu
mbalimbali ili kuongeza mapato ambayo yatasaidia kufanikisha maendeleo
katika sekta mbalimbali.
“Tutajitahidi
kwa kila namna kuwaelimisha wananchi wetu ili wafahamu wajibu wao na
umuhimu katika kulipa kodi na sio kukwepa kulipa kodi na tunawaomba
wananchi kila waendapo kupata huduma yoyote ile iwe katika sekta binafsi
au Serikalini basi anatakiwa aombe stakabadhi za manunuzi au huduma ili
tuweze kudhibiti upotevu wa kodi” alisema Kidata.

Kamishna Kidata aliongeza
kwamba mamlaka hiyo ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na kama
kuna suala lolote au tatizo kuhusu kodi kuna ofisi katika mikoa yote
ikiwa ni hatua ya kutatua shida zao na kama kuna mtumishi yoyote wa
mamlaka hiyo atashindwa kumuhudumia mwanachi inavyotakiwa basi taarifa
zitolewa mara moja kupitia namba zao zilizoko kwenye tovuti ya mamlaka
hiyo, ambayo ni www.tra.go.tz ili kuimarisha huduma zetu kwa wateja.
Aidha
Kamishna Mkuu huyo alisema kuwa watawachukulia hatua wale wote ambao
hawatalipa au hawajalipa kodi zao kwa kuwapeleka mahakamani kwa kukaidi
kulipa kodi halali kwa mujibu wa Sheria.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na ina
mamlaka ya usimamizi wa makusanyo ya Mapato Tanzania na kwa kipindi cha
hivi karibuni kumekuwa na ukwepaji wa kodi uliotokana na sakata la
upotevu wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo kuikosesha
mapato Serikali lakini jitihada thabiti zimefanywa na mamlaka hiyo
kukusanya madeni kutoka kwa wakwepa kodi na kuwafikisha mahakamani ambao
wamekaidi kulipa.a aliongeza

wamekaidi kulipa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )