Ndugu zangu,
Mtakumbuka
kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na
kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni.
Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia
niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook).
Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kuminyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa.
Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania.
Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje.
Niliamini
mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi.
Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa
wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa
na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye.
Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama.
Usemi
wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake.
Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo
wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.
Naomba
mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa
jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi
wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na
nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20.
Niliamua
kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya
jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli
zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko
nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.
Naomba
radhi kwa familia ya baba wa taifa mwalim Nyerere kwa kuitumia kisiasa
siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za
kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )