MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa
Halmashauri za jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya
wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.
Makonda
ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo
ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya
kuapishwa jana.
Makonda
amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za
ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu hivyo lazima matatizo hayo yapate
ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.
Makonda
amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima
wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.
Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.
Makonda
amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala
la ulinzi na usalama kwa wananchi.
Aidha
amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo
la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )