Musa Mateja, Risasi Jumamosi
Dar es Salaam: STAA wa Bongo Fleva
asiyechuja kwa takriban miaka 7 mfululizo, Nasibu Abdul ‘Diamond’
ameeleza mikakati yake kuwa ana mpango wa kumpa mimba nyingine malkia
wake wa nguvu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Risasi Jumamosi
linakuhabarisha.
Diamond ambaye tayari amejaaliwa mtoto
mmoja (Tiffah) na mrembo huyo raia wa Uganda, amefunguka jambo hilo hivi
karibuni alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na mwanahabari wetu kuhusu
mikakati yake ya kimaisha.
Alisema anamshukuru Mungu Zari kukubali kumzalia Tiffah tofauti na warembo wengine aliowahi kutembea nao lakini kwa kuwa yeye anapenda watoto, ameanza ‘kuchakarika’ ili Tiffah apate mdogo wake na si huyo tu, hata na mwingine kadiri Mungu atakavyombariki.
Alisema anamshukuru Mungu Zari kukubali kumzalia Tiffah tofauti na warembo wengine aliowahi kutembea nao lakini kwa kuwa yeye anapenda watoto, ameanza ‘kuchakarika’ ili Tiffah apate mdogo wake na si huyo tu, hata na mwingine kadiri Mungu atakavyombariki.
Nasibu Abdul ‘Diamond’
“Mimi napenda watoto. Bahati nzuri Mungu
pia amenipa mwenzangu ambaye naye anapenda watoto. Hivyo si vibaya
nikifikiria mtoto mwingine na mwingine yani kadiri Mungu
atakavyonijalia.
“Yote hayo nitayafanya kwa utaratibu
maana si unajua tena shughuli zangu za muziki nazo zinanibana, bado
nahitajika nilee familia hivyo nitajipanga vizuri nina imani hakuna
kitakachoharibika,” alisema Diamond.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,
Kabla ya kukutana na Zari, kwa nyakati
tofauti Diamond aliwahi kubanjuka penzini na warembo kama Penniel
Mungwila ‘Penny’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Wema Sepetu ‘Madam’ pasipo
kupata mtoto ambapo staa huyo wa Wimbo wa Utanipenda akisema warembo hao
hawakuwa tayari kumzalia kwa kile alichodai kuwa walizidiwa na nguvu ya
ujana.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )