Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na
kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili
kuwaokoa vijana.
Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina
mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji
anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na
kufuata popote..