Kampuni
ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ilifungua
kesi ya madai ya fidia ya Sh. bilioni 500 Mahakama kuu, kanda ya Dar es
Salaam dhidi ya Zitto Kabwe. IPTL pamoja na wadai wenzake waliiomba
mahakama imwamuru Zitto kulipa fidia hiyo kwa madai ya kutoa kashfa
dhidi yao kimaandishi
Kesi
hiyo dhidi ya Zitto Kabwe na gazeti la Raia Mwema leo imeahirishwa na
Mahakama Kuu ya Tanzania mpaka August 24 2016 baada ya mawakili wa IPTL
kusema shahidi wao muhimu ameumwa ghafla hivyo hataweza kutoa ushahidi.
Katika
kesi hiyo IPTL na mmiliki wake wanadai walipwe Tshs 500,000,000
(Bilioni mia tano) kwa madai kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika
uongo dhidi ya IPTL kuhusu hela zilizoibiwa kwenye Escrow Akaunti.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )