Muimbaji wa ‘Bado’, Harmonize ameteuliwa kuwa balozi wa taasisi
inayojihusisha na utunzaji wa mazingira, World Wide Fund for Nature –
WWF kwa Tanzania.
Muimbaji huyo alisaini mkataba wa ubalozi huo wiki iliyopita kwenye ofisi za taasisi hiyo zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam.
Kama sehemu ya ubalozi huo, Harmonize alihudhuria makabidhiano ya mradi wa maji unaotokana na nishati ya jua huko Kigamboni Jumamosi iliyopita.
Kabla ya Harmonize, ubalozi huo ulienda kwa Rich Mavoko.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )