Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritha Enespher Kabatina ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu
Lucy Fidelis Owenya wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa
viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe
kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa
Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge
Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake ilikuwa ni 110 kati ya
113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane
(8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Uteuzi
wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya
Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka. Vyama
vilivyopata asilimia tano ambayo ilikuwa 780,226 ni.
Na.
|
Jina la Chama
|
Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
|
1.
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
|
8,332,953
|
2.
|
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
|
4,627,923
|
3.
|
Chama cha Wananchi (CUF)
|
1,257,051
|
Baada
ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane (8), Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama
cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano
(5%) ya Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo
vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3
vilivyobaki.
IDADI YA KURA ZA CCM, CHADEMA NA CUF BAADA YA UCHAGUZI WA MAJIMBO NANE (8) KUKAMILIKA
Baada ya kukamilika Uchaguzi katika majimbo nane (8) Idadi ya Kura kwa Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF ni kama ifuatavyo:
Na.
|
Jina la Chama
|
Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
|
Idadi ya Kura baada ya Uchaguzi wa Majimbo nane (8) kukamilika
|
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge.
|
1.
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
|
8,332,953
|
162,535
|
8,495,488
|
2.
|
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
|
4,627,923
|
92,958
|
4,720, 881
|
3.
|
Chama cha Wananchi (CUF)
|
1,257,051
|
17,860
|
1,274,911
|
1.0. MGAWANYO WA VITI VITATU (3) VYA WABUNGE WA VITI MAALUM
Kukamilika
kwa Uchaguzi wa majimbo nane (8) kumeonesha kuwa, Viti vitatu
vilivyosalia vitagawanywa kwenye vyama viwili vya CCM na CHADEMA kwa
mpangilio ufuatao:
CHAM A CHA MAPINDUZI (CCM)
Jumla
ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Mapinduzi ni
8,495,488. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CCM:
Jumla
ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CCM kimepata unazidisha kwa Idadi
ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa
vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge.
Hivyo,
8,495,488 X 113
|
= 66.24 ambayo ni 66
|
14,491,280
|
Hivyo, CCM watakuwa na Viti 66 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 64.
CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla
ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi
ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa
vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge.
Hivyo,
1,274,911 X 113
|
= 9.9 ambayo ni 10
|
14,491,280
|
Hivyo,
CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo
nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge
wa Viti Maalum.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni 4,720, 881. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CHADEMA:
Jumla
ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CHADEMA kimepata unazidisha kwa
Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za
Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali
za Ubunge. Hivyo,
4,720,881 X 113
|
= 36.81 ambayo ni 37
|
14,491,280
|
Hivyo, CHADEMA watakuwa na Viti 37 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 36.
CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla
ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi
ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa
vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge.
Hivyo,
1,274,911 X 113
|
= 9.9 ambayo ni 10
|
14,491,280
|
Hivyo,
CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo
nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge
wa Viti Maalum.
MAPENDEKEZO YA MAJINA YA UTEUZI WA VITI MAALUM KWA VYAMA VYA CCM NA CHADEMA
Tume
hufanya uteuzi kwa kufuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na
Katibu wa Chama husika, kwa mantiki hiyo Tume imewateua Wabunge hao kama
ilivyojitokeza katika orodha za Vyama vya CCM na CHADEMA.
Katika orodha iliyowasilishwa na CCM majina nambari 65 naa 66 ni
65. Ndugu Ritha Enespher Kabati
66.Ndugu Oliver Daniel Semuguruka.
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37 ni
37. Ndugu Lucy Fidelis Owenya.
Asanteni kwa kunisikilizaTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )