Septemba
Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha
ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia
mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.
Leo
March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com na
Fikrapevu.com imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya
wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza
unaolindwa kwa mujibu wa katiba ya Nchi.
Jamii
Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38
cha sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya. Akizungumza kwa niaba
ya Jamii Media,wakili Shukuru Mlwafu ameeleza…
"Baadhi
ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa
na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo
kikatiba.
"Njia
pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu hivyo na kuiomba
mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni batili kwa kuwa
vinaenda kinyume na ibara 16 na 18 ya katiba" Amesema Shukuru Mlwafu
Hatua
hiyo ya kufungua shauri Mahakamani imekuja baada ya kuwepo na
shinikizo kutoka Jeshi la polisi kuwataka Jamii Forum kutoa taarifa za
baadhi ya wateja wake. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Maxence Melo
amesema..
"Kuanzia
uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka
kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa jamii forum kitu
ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na
kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za
wateja, majina halisi na hata maeneo waliopo.Sasa tunaona hii itapekea
kuvunjwa kwa haki ya watumiaji wa Jamii forum":-Amesema Maxence Melo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )