RAIS John Magufuli amemteua Balozi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, kushika nafasi iliyokuwa ikishikwa na Balozi Ombeni Sefue. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, uteuzi huo unaanza mara moja.
Kwa mujibu
wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi huo, Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India akiiwakilisha Tanzania katika nchi za Sri Lanka, Bangladesh, Singapore na Nepal. “Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine”, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo bila kufafanua zaidi.
Rais Magufuli alisifu utendaji wa Balozi Sefue katika kipindi cha miezi mitatu na zaidi, lakini alisema atampangia kazi nyingine. Kijazi aliteuliwa kuwa Balozi wa India mwaka 2013. Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kabla ya kuwa Balozi ikiwamo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi wakati wa utawala wa Awamu ya Nne.
Balozi Sefue aliteuliwa kushika nafasi hiyo mapema mwaka 2012 baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo kumaliza muda wake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )