Waziri
wa Katiba na Sheria Profesa Palamaganda Kabudi amesema majadiliano
yanayofanywa na Serikali pamoja na Kampuni ya Dhahabu ya Barrick kuhusu
mchanga wa dhahabu (makinikia) yamefikia mahali pazuri na kwamba Taifa
litajulishwa hivi karibuni.
Kwa
upande wa Tanzania timu ya majadiliano iliyoundwa na Rais John Magufuli
ilikuwa iliongozwa na Profesa Kabudi wakati timu ya Barrick iliongozwa
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Richard William.
Kamati
hiyo ambayo ilianza majadiliano hayo rasmi Julai 31 mwaka huu ilenga
kujadiliana madai ya Tanzania kwenye biashara ya madini.
Akizungumza
na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya sheria Serikalini mjini hapa,
Kabudi alisema Taifa litataarifiwa kuhusu maendeleo ya majadiliano hayo
hivi karibuni.
“Juzi
na jana tumefikia katika hatua nzuri ambayo nisiseme lakini Taifa
litataarifiwa hivi punde juu ya maendeleo ya utekelezaji wa
tuliyokubaliana,”alisema.
“Baada
ya hapo nilidhani nitapumzika nifanye kazi nyingine lakini mheshimiwa
Rais amenipa jukumu jingine la kusimamia madini ya Tanzanite na Almasi.”
Alisema
shughuli hizo ndizo zimemfanya iwe vigumu kuwatembelea na kuongea nao
tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.
Alisema
miongoni mwa sababu ambayo iliwafanya wasiweke hadharani wajumbe wa
tume hiyo wanaoenda kukutana na kampuni ya Barrick kuepuka watu
kuwachambua kwa faida ya upande wa pili.
Alionya tabia ya wataalam wa sheria kutoa maoni ya kisheria haraka sio nzuri katika kushughulikia maslahi ya Taifa.
“Tutashindwa,
tutalipa fedha nyingi wakati wake si huu. Tutalipa mabilioni ya fedha
tukienda mahakamani. Kwa hiyo alipwe sio wakati wake. Na kwa unyenyekevu
mkubwa tulipoanza majadiliano haya tuliambiwa kuwa Barrick
watawashtaki,”alisema.
“Mtalipa
fedha nyingi, wametushtaki? Nawaulinza nyinyi ndugu zangu wametushtaki
Barrick? Tumelipa hela nyingi? Lakini sio ndio ilikuwa mazungumzo hayo?
Kwamba hapo simesaini (Makubaliano). Subirini mtashtakiwa, mtalipa fedha
nyingi.”
Alisema wengine walisema kuwa Barrick hawatafika katika mazungumzo hayo na kuhoji kama walikuja ama la.
“Mazungumzo
yamevunjika. Sasa mlitaka tuyafanye hadharani? Moja ya sababu ya wale
kufichwa isipokuwa mimi nifahamike wala ilikuwa hatuwaogopi sana wale.
Nyinyi Watanzania maana mngeanza kuchambua huyu darasa la nne
alifeli,”alisema.
“Kwa
hiyo mngeanza kuchambua watu kwa faida ya yule (Barrick) badala ya
kupeana. Hatukukutana na watu wadogo. Jana tulikuwa na Richard Willison
(Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick… komandoo yule (Willison)
lakini pamoja na ukomandoo wake si tulipambana naye bwana?”
Alisema
ni lazima kusimamia maslahi ya Serikali bila woga wowote na kwamba
inakera kusikia mwanasheria akisema kesi ni ngumu nakwamba Serikali
ilipe fedha haraka sana.
“Tutashtakiwa
sasa wewe umeajiriwa kwasababu gani? Si uende upambane. Nasema hili
mjue nyakati zimebadilika. Mjiulize zimepitishwa sheria mnazifahamu
zilizopitishwa si za wizara yako?”alihoji.
Pia
alisema kuwa kwa muda wote wa majadiliano ya makinikia wajumbe wa timu
hiyo hawakukaa majumbani kwao kutokana na uhalisiana wa suala hilo.
Profesa
Kabudi alisema majadiliano kuhusu mkataba kati ya Serikali na Kampuni
ya upakuaji makontena bandarini ya Tanzania (TICTS) yamewezesha kampuni
hiyo kuongeza mapato.
“Tulifanikiwa
kukaa na wale wa Hong Kong na kufanikiwa kuubadilisha mkataba ule mara
ya kwanza ulikuwa ni mkataba ambao kwa mwaka kodi ya pango ni dola
milioni 7 lakini sasa ni dola milioni 14 zinazoongezeka kwa asilimia
tatu kila mwaka,”alisema.
Alisema fedha hizo zitalippwa mwanzo wa mwaka zote na kwamba mwaka huu wamelipa dola za kimarekani milioni 17.3
Alisema anza kutoa Dola za Marekani milioni 14 kila mwaka badala ya dola za marekani milioni 7 kila mwaka kama kodi ya pango.
Alisema awali mkataba ulikuwa hautoi nafasi ya kuongeza kodi sasa unatoa ongezeko la asilimia la asilimia tatu.
“Tumekubaliana
wawe wanalipa kwa mkupuo mwanzo wa mwaka wa fedha na Julai mwaka huu
badala ya kulipa oktoba wamelipa Dola za marekani milioni 17.3,”alisema
Kabudi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )