Leo
January 16, 2018 wafanyabiashara wawili Kalrav Patel na Kamal Ashar
wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutumikia miaka 2 jela
au kulipa faini ya Sh.milioni 64, ambapo pia wametakiwa kulipa
Sh.Milioni 694 baada ya kuisababishia hasara TCRA.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema
mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao katika makosa saba
yanayowakabili.
Hakimu
Mashauri amesema katika kosa la kwanza la kula njama, washtakiwa
wanahukumiwa kwenda jela miezi 12 ama kulipa faini ya Sh.milioni 2 kwa
kila mmoja.
Pia
katika kosa la pili hadi la saba, Hakimu Mashauri amesema washtakiwa
hao wamehukumiwa kwenda jela miaka 2 ama kulipa faini ya Sh.milioni 5
kwa kila mmoja.
Pia
Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo inawaamuru washtakiwa hao kulipa
Sh.Milioni 694 ikiwa ni fedha zinazotokana na hasara waliyoisababisha
kwa TCRA.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )