JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Ami Lukule,
anayedaiwa kuwaua mke na mtoto wake kichanga cha umri wa miezi minane na
mdogo wake wa kike, katika eneo la Matosa Darajani, Goba wilaya ya
Kinodnini jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita.
Akizungumza
na wanahabari leo Januari 16, 2017 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumya Dar, Lazaro Mambosasa amemsema mtuhumiwa huyo
alikamatwa hivi karibuni mkoani Iringa.
“Mtuhumiwa
huyo tayari tumeshamkamata na baada ya kumhoji alikiri kufanya tukio
hilo na kusema chanzo alikuwa mtoto. Amedai mkewe huyo alimtilia mashaka
kwa kuingia kwenye mahusiano na mwanammme mwingine, anadai mke huyo
alimzalia mtoto nje ya ndoa, hivyo akaamua kumnyonga mtoto na kufanya
mauaji mengine mliyoyasikia,” alisema Mambosasa.
Aidha,
Kamanda Mambosasa amesema kwa sasa wanafanya taratibu za kumsafirisha
mtuhumiwa huyo kutoka Iringa hadi Dar ili kufikishwa mahakamani.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )