Madereva
watatu wa malori yaendayo mikoani na wasaidizi wao watatu, wamenusurika
kifo baada ya kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwilini na mlinzi wa
nyumba moja ya wageni iliyopo Ubena, Chalinze mkoani Pwani.
Tukio
hilo limetokea jana alfajiri saa 11.30 kwenye hoteli hiyo ambako
madereva na wasaidizi hao walikuwa wamefikia kwa mapumziko kabla ya
kuendelea na safari.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventura Mushongi alisema tukio hilo
lilitokea baada ya kuwapo kutokuelewana kati ya mmoja wa madereva na
mlinzi wa nyumba hiyo.
Kamanda
Mushongi alisema taarifa za awali zinasema baada ya mabishano hayo
ambayo bado hayajajulikana chanzo chake, mlinzi huyo alikoki silaha yake
aina ya Shortgun na kupiga risasi moja hewani kutuliza vurugu na
kumjeruhi mmoja wa madereva hao.
Hata
hivyo, mabishano yalizidi baada ya madereva wengine kujitokeza
kuingilia ndipo mlinzi huyo akapiga risasi nyingine ambayo ilitoka na
gololi zake kusambaa na kuwajeruhi wengine wanne ambao walipelekwa Kituo
cha Afya Chalinze kwa matibabu.
Alisema mlinzi huyo amekimbia na anaendelea kutafutwa na chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Chalinze, Dk Victor Bamba alisema walipokea
majeruhi watano ambao walipatiwa huduma ya kwanza na kutokana na hali
zao kuwa mbaya walihamishiwa Hospitali ya Tumbi.
Akizungumza
wodini Tumbi walikolazwa, mmoja wa madereva hao, Harun Adeli alisema
walifika hapo juzi saa mbili usiku na kuamua kulala ndani ya magari yao
ili jana waendelee na safari na ilipofika saa kumi na moja alfajiri
walisikia makelele yanayoashiria ugomvi ndani ya hoteli hiyo.
“Wakati tunashangaa tulishtukia risasi zinarindima na ndipo zilipotufikia,” alisema.
Muuguzi
wa zamu katika Hospitali ya Tumbi, Habibu Yahaya alisema aliwapokea
majeruhi Stephen Fredy, Beno Henry, Akrey Dallu, Ramadhani Saidi, Amani
Almasi na Adel wote wakazi wa Dar es Salaam.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )