Labda
ukweli unauma.. Kwamba wengi tunatamani sana maisha mazuri anayoishi
Diamond na mchumba wake, Zari the Bosslady. Wapo wanaoishia kutamani na
kumuomba Mungu nao waje kuwa na maisha hayo, wengine hushukuru na
hufurahi tu kwa kile walichonacho ama tumeseme wameridhika na kidogo
wanachopata.
Lakini
wapo ambao hushindwa kujizuia kupata wivu na kuwachukia tu watu wenye
mafanikio – wa kuitwa haters. Hayo ni majaribu makubwa waliyonayo mastaa
duniani. Lakini sio mara zote huvumilia matusi na kejeli wanazozipata
kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati
Zari akiendelea kula raha Ulaya na mchumba wake Diamond, ameendelea
kutupiwa vijembe na watu kuwa hawajali tena wanae watatu aliowaacha
Afrika Kusini, kwamba kila siku kiguu na njia na Diamond. Hilo
limemkera, na ameamua kulijibu.
Staa huyo amepost picha hiyo juu na tafsiri yake kwa maneno hayo ni:
Watoto
wangu wameniuliza, kwanini kila mtu amechukia? Nimewaambia tuna vitu
ambavyo hawana. Wakati mnachukua, mimi naenda mall, kumwaga fedha.
Naweza, huwezi
Lakini
pia aliweka caption isemayo: Baadhi yenu hamtaelewa hili lakini ni
sawa. Ninawajibika kwa ninachoandika, na sio unavyokielewa.
Hilo limeonakana kuwakera wengi, wakiwemo mashabiki wake. Baadhi waliongea mambo mazito kiasi cha kumfanya awajibu pia.
Well,
good news ni kubwa ex wake, Ivan, amewachukua wanae na kuwapeleka
kwenye kisiwa cha maraha cha Ibiza kula pizaa! So waswahili wanasema
hiyo ni ngoma drooo… Pesa inaongea!!
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )