Naibu
Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla jana alitumia dakika kadhaa kutoa
ufafanuzi kwa wabunge kuhusu tofauti iliyopo kati ya dawa za kulevya
aina ya bangi na pombe kali za viroba.
Alisema pombe yenye kilevi kilichothibitishwa haiwezi kuathiri afya ya mtumiaji kama ilivyo dawa ya kulevya.
Ufafanuzi
huo ulitokana na swali la Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya maswala ya
Ukimwi,Mohammed Amour aliyetaka kujua tofauti ya kitaalamu baina ya
bangi na kiroba kutokana na jinsi zinavyowatesa watumiaji.
Mbunge
huyo wa Bumbwini Unguja alisema kuna kiwango kikubwa cha kilevi
kilichopo katika viroba kinachoweza kusababisha athari kwa watumiaji.
Akizungumza
na wajumbe wa kamati hiyo kwenye ofisi ya wakala wa maabara ya mkemia
mkuu wa serikali, Dr. Kigwangalla alisema: "Madhara yanatofautina, ya
muda mrefu na ya muda mfupi.Utumiaji wa bangi unaathiri mfumo wa
fahamu kwenye ubongo, lakini pombe iliyopimwa kiasi cha alkoholi haiwezi
kukuathiri."
Licha
ya majibu hayo,Dr. Kigwangalla aliahidi kufuatilia suala hilo katika
mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo inahusika na vipimo
kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
"Nitafuatilia
kwa kina TFDA nione wanafanyaje, kwa nini viroba vimekuwa vikiuzwa
mitaani tofauti na viwango halisi vya alkoholi." Alisema
Awali,
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alisema wafanyabiashara
wa viroba wamekuwa wakitumia ujanja wa kuweka nembo ya asilimia ndogo
lakini uhalisia wa kiwango cha alkoholi katika kiroba chenyewe ni
kikubwa zaidi.
“Wanabandika asilimia sita kumbe ni asilimia hata 30 ya alkoholi.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )