MWIGIZAJI wa filamu Hemed Suleiman ‘Phd’ anatafutwa na mtayarishaji wa Filamu nchini baada ya kuchukua malipo kwa ajili ya kushiriki filamu ya Maziko saa sita na kulala mitini FC imetonywa na mdaku aliyopo anga za Phd anazopinda kujidai.
Mdaku huyo akiidakisha FC amedai kuwa msanii huyo wa muziki na filamu huku akifanya poa katika filamu kuliko muziki amejikuta akimpatia Bi mkubwa wake kibarua kisicho na malipo kwa kuulizwa kila uchwao alipojificha na mtayarishaji huyo.
Mtaayrishaji wa filamu hiyo ya Maziko saa sita Ndugu Thomas Simon Koga almaarufu kama Koga Roho sita amefunguka kwa kusema kuwa toka mwezi wa sita Hemed alilipwa kiasi cha milioni moja na nusu kwa ajili ya kuigiza filamu hiyo lakini hadi leo hapatikani.
“Wasanii hawa wakubwa baadhi yao wanatusumbua kweli leo ni miezi kadhaa sasa toka niimlipe Hemed kwa ajili ya kazi yangu lakini amekimbia simu hazipatikani kila siku mimi kiguu na njia kwa Bi. Mkubwa wake,”anasema Koga.
Jana siku ya jumapili Koga alionana na mama yake mzazi wa Hemed na kumweleza kuwa anampa siku moja awe ameonekana na kurudisha fedha au kushiriki katika filamu kama walivyokubaliana, kwa mara ya kwanza Phd kutoka mafichoni akampigia simu.
Akidai kuwa anamtishia kama anataka kumkamata hivyo basi ampe nafasi hadi siku ya Jumanne atamalizana naye kwa kumalizia scene zilizobaki, FC ilimtafuta Hemed kwa njia ya simu bila mafanikio.
Kesi za mfano huu zimekuwa nyingi sana hasa kwa watayarishaji wasio na majina pale wanapoambiwa na wasambazaji lazima sinema ili nisambaze awepo msanii Fulani ndipo wasanii tajwa uwasumbua kwa kuchukua fedha na kulala mitini.
Ripoti na Filamucentral
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )