Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu
taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la
Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu
shakani”.
Taarifa
hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa
Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi
iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia
trilioni 2.17 una mashaka.
TPDC
inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika
kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015.
Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo:
1.
Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo
kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo
vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”
2.
Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima
“pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa
gesi
3. Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine.
Baada
ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya
Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na
pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama
mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo.
Taarifa
hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi
ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF).
Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa.
Kwa
kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi
katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa
ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa
trilioni 2.17.
Mkandarasi
atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa
kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal
program”.
Mnamo
Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu
kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi
kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na
65.
Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )